Mgombea wa nafasi ya urais kupitia tiketi ya Republican, Donald Trump ameanza kuonyesha wasiwasi wake kuwa huenda uchaguzi mkuu wa mwezi Novemba mwaka huu ukagubikwa na wizi wa kura.

Akiongea na maelfu ya wafuasi wake kwenye eneo la Columbus, Ohio, amesema amesikia ‘zaidi na zaidi’ kuwa uchaguzi hautakuwa wa haki lakini akashindwa kutoa ushahidi wa papo kwa hapo kuthibitisha kauli hiyo.

Kama hiyo haitoshi, Trump amemwita mpinzani wake kwenye uchaguzi huo, Hillary Clinton wa Democratic ‘Shetani’kumshambulia kwa maneno mama wa mwanajeshi wa kiislam aliyeuawa vitani nchini Iraq, Ghazala Khan alipokuwa jukwaani na baba wa kijana huyo Khizr Khan katika kumpigia kampeni mgombea urais kwa tiketi ya Democratic, Hillary Clinton.

Kuhusu uchaguzi mkuu ujao, Trump amekaririwa akisema: ‘Nina wasiwasi kuwa uchaguzi ujao utakumbwa na wizi, lazina niwe mkweli’.

Baadae tena akayarudia maneno yake kupitia kituo cha televisheni cha Fox kwa kusema ‘Nadhani chama cha Republican kinafuatilia jambo hili kwa makini sana vinginevyo tutapokonywa ushindi wetu’.

Trump aliwahi kutoa kauli kama hizo wakati wa kinyang’anyiro cha chama cha Republican kuwania nafasi ya kuteuliwa kuwania nafasi hiyo.

Wachambuzi wa mambo wamedai kuwa Trump anatafuta kuungwa mkono na wapiga kura wasiokuwa na imani au anatafuta njia ya ‘kutorokea’ matokeo yakiwa mabaya upande wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *