Rais wa Marekani,  Donald Trump amewasili nchini Korea ya Kusini kwa ziara ya kikazi ya mashariki mwa bara la Asia ambapo atatembelea nchi tano.

 Trump alikuwa akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari na mwenzake wa Korea Kusini Moon Jae-in mjini Seoul kama sehemu ya ziara yake barani Asia.

Mapema Trump alikuwa ametishia hatua kali za kijeshi dhidi ya Korea Kaskazini.

Yuko kwenye ziara ya nchi tano barani Asia ambapo programu za nyuklia za Korea Kaskazini zimekuwa kwenye ajenga.

Trump na Moon walirejelea wito wao kwa Korea Kaskazini kuachana na mipango yake ya nyuklia akisema kuwa ni jambo bora kwa Korea Kaskazini kuja kwa mazungumzo.

Licha ya Marekani kupeleka wanajeshi wengi eneo hilo, Trump alisema kuwa ana matumaini kwa Mungu kuwa hatachukua hatua za kijeshi dhidi ya Korea Kaskazini.

Trump pia alisema kuwa Korea Kusini itaagiza vifaa vya kijeshi kutoka Korea Kaskazinia vya gharama ya mabilioni ya dola.

Haijulikani ikiwa makubaliano hayo tayari yalikuwa yameafikiwa lakini Moon alisema kuwa walikuwa wamekubaliana kuanza mazunguznoa hayo ili kuboresha uwezo wa ulinzi wa Korea Kusini.

Licha kuwa Trump atakuwa nchini Korea Kusini kwa muda wa saa 24, itakuwa ziara muhimu zaidi kwa nchi hizo zote anazozuru barani Asia.

Ziara hiyo ina lengo la kuboresha ushirikiano wa kijeshi ambao umeilinda kwa muda mrefu Korea Kaskazini na ndio ujumbe wanaotaka kutuma kwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *