Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari leo amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na  Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu kukabiliana na ugaidi nchini Nigeria.

Buhari ambaye yuko mjini London kwa ajili ya matibabu amempongeza Trump kwa kuchaguliwa kuwa rais wa Marekani kwenye uchaguzi wa Marekani uliofanyika mwaka jana.

Viongozi hao wawili walizungumzia njia za kuboresha ushirikiano katika vita dhidi ya ugaidi unaosababishwa na makundi mbali mbali katika nchi hizo.

Rais Trump amemshauri Rais Buhari kuendelea na kazi nzuri anayoifanya na pia kampongeza kwa jitihada alizofanya za kuokoa wasichana 24 wa Chibok na hatua zinazopigwa na jeshi la Nigeria.

Pia Trump amemhakikishia rais huyo wa Nigeria kuwa Marekani iko tayari kuafikiana na Nigeria kuhusu suala la kuisaidia na silaha ili iweze kukabiliana na ugaidi nchini humo.

Mwisho wa maongezi hayo Rais Trump amemualika Buhari kufanya ziara nchini Marekani atakaporejea nchini kwao kutoka Uingereza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *