Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuna uwezekano mkubwa kupatikana kwa amani mashariki ya kati katika mazungumzo na rais wa Palestina Mahmoud Abbas.

Kwa upande wa Rais wa Palestina Mahmoud Abbas alimuambia Trump katika ikulu ya Whitehouse kwamba anataka kuwepo kwa makubaliano ya amani ya mpango wa kudumu wa mataifa mawili yalio huru ikiwemo mipaka iliokuwepo kabla ya 1967.

Hat ahivyo bwana Trump amekuwa na mawazo tofauti kuhusiana na utatuzi wa mataifa mawili yalio huru.

Mnamo mwezi Februari alisema kuwa anachukulia swala la taifa moja na mataifa mawili yalio huru na napenda wazo ambalo linaungwa mkono na mataifa yote mawili.

Siku ya Jumatano, rais huyo wa Marekani alisistiza kwamba hakutakuwa na amani ya kudumu hadi mataifa yote mawili yatakapopata njia ya kusitisha uchochezi wa ghasia.

Kiongozi huyo wa Palestina anashinikizwa kusitisha malipo kwa familia za wafungwa wa Kipalestina pamoja na zile za wale waliouawa katika mzozo dhidi ya Israel.

Serikali ya Israel inasema kuwa malipo hayo yanachochea ugaidi, lakini maafisa wa Palestina wanasema kuwa kusitisha malipo hayo itakuwa pigo la kisiasa kwa rais Abbas ambaye hana umaarufu mkubwa nyumbani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *