Mhudumu wa bar amfungulia mashtaka Trey songz kwa tuhuma za kumpiga mnamo Mei 9,2019 huko Hollywood Palladium na kumsababishia matatizo ya kiafya, ikiwemo kuathirika kisaikolojia na maumivu makali hivyo amefungua shauri kudai fidia.

Taarifa zinasema kuwa star huyo wa R&B alikataa kufuata utaratibu wa kutokukaa kwenye bar hiyo wakati onesho la mavazi “Fashion Nova” likiendelea kwenye ukumbi huo uliokuwa karibu na Bar.

Mhudumu alimfuata Trey Songz na kumgusa begani ili aondoke eneo lile lakini ilikuwa tofauti kwani Trey songz aligeuka na kumpiga kichwani, kisha aliendelea kutazama onesho lililokuwa likiendelea wakati huo.

Ikumbukwe kuwa zimepita siku kadhaa tu tangu shauri lake liondolewe kutokana na kutojitosheleza kwa ushadi wa tukio alilolifanya Januari 24,2021 huko Kansas City kwenye mchezo wa playoff kati ya Kansas dhidi ya Bills la kumdharirisha askari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *