Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) imefunga ofisi za kampuni ya Sahara Media Group inayomiliki vituo vya Radio Free Afrika na Star Tv kutokana na deni la shilingi bilioni 4.5.
Ofisi hizo zimefungwa leo na wakala wa TRA, Kampuni ya Sukah Action Mart and Court Brokers ya jijini Mwanza.
TRA imewamewaondoa studio wafanyakazi wote na kuifunga radio hiyo. Kwa sasa ukiwasha radio utasikia matangazo ya kiingereza ya BBC.
Meneja utumishi na utawala wa Sahara Media Group, Raphael Shilatu amesema ni kweli ofisi hizo zimefungwa kutokana na malimbikizi ya madeni yanayotokana na kuhama kutokan mfumo analogia kwenda digitali.