Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Bank ya Uwekezaji Tanzania ‘TIB’ zimesaini Mkataba kwa lengo la bank hiyo kusaidia katika shughuli ya ukusanyaji kodi mbalimbali zinazotozwa na TRA.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Charles Kichere amesema kuwa wamesaini mktaba na TIB ili kuwasiadia katika shughuli ya ukusanyaji wa kodi.
Pia amesema kuwa TIB itawasadia kukusanya kodi zinazotozwa na Mamlaka hiyo ikiwa ni kutekeleza agizo la Rais Magufuli la kuitaka TRA kufanya kazi saa 24 Bandarini.
Kichere amesema kuwa TRA ina mfumo wake wa kutoza kodi ambao hushirikisha mabenki mbalimbali nchini katika mfumo unaoujulikana kama Taxi Bank ambapo baada ya walipa kodi kutumia mfumo huo kufanya malipo, malipo hayo huenda moja kwa moja kwa TRA.