Vituo vya kuuza dizeli, petroli na mafuta ya taa vimeendelea kufungwa nchini kutokana na kutokuwa na mashine za kielektroniki za kutoa risiti (EFDs).
Hatua hiyo inayotekelezwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imeelezwa kuwaathiri si tu wenye vituo bali hata watumiaji.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo amesema leo na kuongeza kwamba wanaendelea na kazi hiyo nchi nzima ili kuhakikisha sheria inatekelezwa.
Kayombo amesema kuwa zoezi hilo ni endelevu mpaka pale watakapotii agizo la kutumia mashine hizo za kielektroniki.
Hatua hiyo imekuja kufuatia baadhi ya vito vya kuuzia mafuta nchini kutotii agizo la kutumia mashine za EFD’s.