Mamlaka ya Mapato nchini TRA imesema kuwahaitaongeza muda wa zoezi la uhakiki wa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi kwa jiji la Dar es Salaam.

Hiyo ni baada ya muda wa kufanya hivyo kufikia ukomo hii leo na kwamba wale watakaoshindwa kufanya hivyo watatakiwa wawasiliane na mameneja wa TRA wa mikoa husika.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Bw. Richard Kayombo, ametoa msimamo huo wa TRA jijini Dar es Salaam leo huku akiweka wazi kuwa ni kosa kwa mtu yoyote kufanya biashara kwa kutumia TIN namba ya zamani.

Katika baadhi ya ofisi za TRA, jeshi la polisi limelazimika kuimarisha ulinzi kutokana na msongamano wa watu wanaosubiri huduma  hiyo ya uhakiki wa TIN namba ambapo baadhi ya waliohojiwa wameiomba TRA ibadili msimamo wake na kuongeza siku ili kukamilisha zoezi hilo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *