Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imepokea boti mbili za kisasa za kuongozea meli ambazo zitatumika katika Bandari ya Dar es Salaam na Tanga.
Meneja Mawasiliano wa TPA, Janeth Ruzangi amesema kuwa ujio wa boti hizo kutoka China utasaidia kuongeza kasi ya utendaji kazi katika bandari na kuongeza ufanisi.
Meneja ameongeza kwa kusema vyombo hivyo vya majini vimeletwa ili kuboresha huduma na kuleta ufanisi bandarini.
Pia amesema ujio wa vyombo hivyo ni sehemu ya mkakati maalumu wa TPA katika kuongeza vitendea kazi upande wa majini na nchi kavu ili kuongeza kasi ya upakuaji na upakiaji wa mizigo.