Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imesema itawachukulia hatua watumishi wa mamlaka hiyo wote ambayo wanajishughulisha na michezo michafu wakishirikiana na wafanyabiashara katika minada inayofanyika bandarini.

Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Deusdedit Kakoko amesema hatua ambazo atachukua ni pamoja na kupiga mnada mali za wahusika wote ambao watabainika kuhusika katika mchezo huo mchafu.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa hiyo ambaye ni mdau wa bandari, kuna ujanja unaofanywa na baadhi ya wafanyakazi ambao wanaagiza mzigo kutoka nje, wanalipia asilimia chache kwa makubaliano kwamba mzigo huo utakapofika bandari ya Dar es Salaam atamalizia fedha zilizobaki.

Lakini wafanyabiashara hao matokeo yake wakifikisha mzigo hapa nchini badala ya kulipa fedha zilizobaki wanachelewesha kulipia mzigo mpaka muda unapita wa kuhifadhi mzigo bandarini na mzigo huo kupigwa mnada.

Aidha, mchezo huo mchafu hufanywa na wafanyakazi wasio waaminifu wa TPA kwa kushirikiana na wafanyabiashara kisha mzio anauziwa kwa bei ya chini ambapo bila kulipa fedha ambayo mfanyabiashara alikuwa amebakiza deni alikochukulia mzigo jambo ambalo linachafua jina la bandari ya Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *