Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Tommy Flavour amefunguka na kuthibitisha kuwa anatarajia kuachia albam yake mpya mapema mwezi huu.

Tommy Flavour ameweka Wazi Ujio Wa Album Yake Mpya Ambapo Ameeleza Kwa Anaiachia Ndani Ya Mwezi Huu baada ya kukamilika kwa albam hiyo.

”Album yangu ipo na muda wote ambao nilikuwa kimya nimekuwa nikiiandaa na kuiboresha na kwa dua zangu na management yangu tulipanga mwezi huu wa pili tutaitoa album yangu” Amesem.

Tommy ambaye yupo chini ya lebo ya King’s Music hii itakuwa albam yake ya kwanza kuachia toka alipoanza muziki chini ya lebo hiyo inayoongoza na Alikiba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *