Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari dhidi ya mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha katika baadhi ya maeneo nchini kuanzia leo Alhamisi na kesho Ijumaa.
Kwenye tarifa iliyotolewa leo na Mamlaka hiyo imesema mikoa ambayop itaathirika na mvua hizo ni pamoja na Pwani ya Kusini ambayo ni Lindi na Mtwara, Nyanda za Juu Kusini Magharibi ambayo ni Mbeya, Iringa, Songwe na Rukwa, Dar es Salaam na Pwani.
Taarifa hiyo imeeleza kwamba upepo wa Pwani, unatarajiwa kuvuma kutoka Kaskazini kwa kasi ya Km 30 kwa saa kwa Pwani ya Kaskazini na kwa kasi ya km 20 kwa saa kwa Pwani ya Kusini.
Pia hali ya bahari inatarajiwa kuwa mawimbi madogo hadi makubwa kiasi, na matazamio kwa siku ya Ijumaa Januari 5, 2018 kutakuwa na kuongezeka kwa mvua katika mwambao wa Pwani na maeneo ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi.