Msanii Mkongwe wa Bongo Fleva, Khalid Mohamed ‘TID’ amesema kuwa wasanii wengi nchini wanaoa kwa kutafuta kiki ila kwa upande wake hawezi kufanya hivyo.

Ameyasema hayo baada ya kupita takribani siku 24 tokea msanii huyo kutangaza wazi kuwa yupo katika mahusiano na mwanadada mmoja ambae alikuwa nae nchini Ujerumani jambo ambalo wengi walitarajia akitangaza ndoa siku chache zijazo.

 

Amesema kuwa ‘Unajua sasa hivi watu wanataka kutengenezea kama kiki kitendo cha kuoa, kwa hiyo mimi sio mtu kutafuta kiki kwa kutumia ndoa,”.

 

Pia TID amesema kuwa Q-Chief alishawahi kutangaza kutaka kuoa lakini mpaka sasa hakuna chochote alichokifanya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *