Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Khalid Mohamed maarufu kama T.I.D amefunguka na kusema kuwa wanamuziki wanaoachia nyimbo mfululizo waroho wa kutaka kujulikana wenyewe kwenye ulimwengu wa muziki.
T.I.D amesema kuwa wasanii wanaotoa nyimbo kila siku ni washamba, hwajiamini na wana uroho wa kutaka kusikilizwa.
Kwenye Mahojiano hayo T.I.D alifunguka yafuatayo:
Amesema kuwa “To me ukiniambia kutoa nyimbo nyingi kwa wakati mmoja I don’t think kwamba ni kitu cha maana kwanza msanii unakuwa unajiangusha kwasababu in one way or another humpatii mtu nafasi, hapa sio Marekani huko mziki ni kazi kubwa sana people have a lot of time technology kwao imefika mda mrefu alafu wapo wengi kiasi cha kwamba unaweza ukatoa nyimbo mbili kwa wakati mfupi.
Kumekuwa na mjadala mkubwa Kama ni sawa kwa msanii kutoa nyimbo mara kwa mara au wasubiri muda mrefu, msanii Kama Diamond anasifika kwa kutoa nyimbo zake kila baada ya muda mfupi lakini Alikiba hukaa muda mrefu halafu huja kutoa nyimbo zake.