Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Khalid Mohamed maarufu kama TID amesema kuwa amehuzunika sana kwa baadhi ya vyama kutumia msemo wake wa ‘Ni yeye’ kwenye kampeni zao za kisiasa.
TID ambaye alitamba na wimbo wa Zeze miaka hiyo amedai kuwa msemo huo ulikuwa ni maalum kwa Rais John Pombe Magufuli tu lakini siyo kwa wanasiasa wengine.
Mwanamuziki huyo amesema ameumizwa sana na kitendo hicho kwa sababu amekuwa akitumia akili yake na ubunifu wa kufikiria wazo la msemo huo, hivyo anaona kama anadhulumiwa na kutaka haki itendeke juu ya suala hilo.
TID amesema kuwa “Nimehuzinuka sana na nimeona kwenye mitandao ya kijamii kuwa msemo wangu, ushairi wangu na ubunifu wangu unatumika kwenye kampeni za kisiasa bila ya kuwa na mawasiliano yoyote.
Pia TID amewajumuisha kwenye posti yake Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Juliana Shonza, Katibu wa Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole, Mwana Fa , na Cosota chombo ambacho kinasimamia haki miliki za wasanii.