Mwanamuziki wa Bongo Fleva, TID amesema kuwa kuna baadhi ya vyombo vya habari (media) ambazo ziligoma kupiga muziki wake kwa lengo la kuzima kipaji chake.

TID amesema kwamba, licha ya changamoto hizo ameendelea kufanya vizuri katika muziki wa Bongo Fleva.

Vile vile amesema kwamba hulka yake ya kukosoa vituo vingi vya habari kuhusu namna ya kuendesha mambo yao, ilimchonganisha na watu wengi, jambo ambalo lilimsababishia kupoteza pesa nyingi ambazo angezipata kupitia muziki wake.

TID amesema licha ya kukosa kupanda jukwaani kwa muda mrefu, alifanikiwa kutafuta mbinu na biashara mbadala za kuleta chakula mezani, jambo ambalo anaamini linazidi kumfanya awe kidedea kwenye gemu la Bongo.

TID anaweka wazi kwamba kuna asilimia kubwa ya wasanii ambao amewashika mkono na hata kuwakutanisha na wasanii wakubwa ili washirikiane kwenye kazi za kimuziki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *