Waziri mkuu wa Uingereza, Theresa May amehudhuria mkutano wa Umoja wa Ulaya nchini Ubelgiji ikiwa ni mara yake ya kwanza toka aingie madarakani baada ya kujiuzuru David Cameron.

May amesema atawaambia wenzake kwamba Uingereza itatoa mchango wake kikamilifu hadi kuondoka kwake, na utakuwa imara na wenye kutegemea washirika baadae.

Kwa upande wake rais wa Ufaransa, Francois Hollande ameonya kuwa kama Bi May alitaka kujiondoa kikamilifu katika Umoja wa ulaya kungekuwa vigumu kukubaliana katika miezi ya mbeleni.

Taarifa zimesema serikali ya Bi May ina mgawanyiko juu ya biashara gani Uingereza inapaswa kulenga.

Uingereza inatarajiwa kuanza mchakato wa kujiondoa rasmi mwishoni mwa mwezi Machi mwaka ujao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *