Waswahili wana msemo wao ‘Mambo ya ngomani huishia ngomani’………Msemo huu kwa ujumla wake unafundisha juu ya hekima ya kumaliza tofauti au mambo yasiyoridhisha ambayo mtu anaweza kuyapitia kwenye maisha yake (bila kutarajia) kisha akatamani mno kuyaeleza hadharani ili kupata msaada (wakati mwingine si msaada wa kutatua tatizo husika bali msaada wa kuona sura ya anayeambiwa ikiendana na kile anachokitaka yeye).

Msemo huu ni msemo muhimu sana kuzingatiwa katika zama hizi ambazo utandawazi umeifikisha dunia kwenye sehemu ambayo watu hata wasiowafahamu watu kwa sura huweza kuyafahamu mambo ya watu hao kwa upana sana na kupelekea fedheha au matatizo zaidi.

Tatizo la aina hii limeendelea kuisumbua industry ya burudani ya Tanzania ambapo wadau wa tasnia hiyo wamekuwa wakidhihirisha mambo waliyoyakubaliana aukuyafanya kwa siri wakiwa peke yao pindi zinapotokea tofauti baina ya watu hao. Je, tasnia hii itakua zaidi ikiwa makosa aidha madogo au makubwa (ya kitasnia) ambayo yanaweza kurekebishwa au tofauti zinapojitokeza zinaweza kurekebishwa yanapowekwa hadharani na kuvutia mijadala mikubwa isiyochunga mipaka ya wachangiaji wala mipaka ya lugha itayotumika?

Wadau wa sanaa Bongo tumieni busara kwenye kumaliza tofauti zenu ‘kimya kimya’ ili kweli msimame kwenye hadhi ya kuwa ‘kioo cha jamii’.

We would like to humbly ask all the entertainment industry stars including director Nisher and rapper G-Nako who are currently in ‘AROSTO’ video feud to resolve their disputes in privacy. Social media only add fuel to burning issues.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *