Shirikisho la soka Tanzania (TFF) limepiga marufuku watu kuingiza siasa katika mchezo wa leo kati ya Simba na Yanga.

Afisa Habari wa TFF, Alfred Lucas amesema kuwa wamepata taarifa kuna baadhi ya mashabiki leo wanataka kuchana kadi za chama fulani, wengine wanataka kuchoma bendera za chama fulani kupitia mchezo wa leo kati ya Simba na Yanga.

Lucas amesema kuwa ni kosa kwenye mpira wa miguu kuingiza siasa kwenye michezo na kusema kwa yoyote atakayejaribu adhabu kali itachukuliwa dhidi yake.

Amesema kuwa “Kuna watu tumesikia na kuthibitishiwa kwamba kuna watu leo wanataka kuchana kadi za chama fulani cha siasa uwanja wa Taifa mbele ya mashabiki wa Simba na Yanga, kuna wengine wamepanga kuzichoma moto, wako wale wengine

Pia ameongeza kwa kusema kuwa “wamepanga kuchoma hata bendera za chama hicho, wengine wanasema watafanya ndani ya uwanja wengine nje ya uwanja, nitumie nafasi hii kuwaambia kwamba taarifa tunazo na tunatoa onyo kali kwa yoyote atakaye thubuti kufanya hayo wanayotaka kufanya kwani litakalo mtokea lisijekuwa lawama kwa TFF.

 

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *