Klabu ya Arsenal wako tayari kumsaini kiungo wa kati wa Manchester United, Henrikh Mkhitaryan kama sehemu ya makubaliano ya kumsajili mshambuliaji Alexis Sanchez.
Arsenal ilifanya mazungumzo na mshambuliaji wa Bordeaux Malcom siku ya Jumapili na wanatarajia kulipa pauni milioni 40 kwa mBrazil huyo wa miaka 20.
Chelsea bado wako katika mikakati ya kumsaini mshambuliaji wa mwezi Januari kwa mkopo huku Andy Carroll wa West Ham akiwa katika nafasi nzuri wa kusainiwa.
Manchester United wako tayari kumpa kipa wa miaka 27 David de Gea mkataba mpya amboa utamweka katika klabu hiyo katika taaluma yake yote.
Crystal Palace wana matumaini ya kumaliza kumsaini mshambuliaji wa Fiorentina raia wa Senegal Khouma Babacar 24 kwa pauni milioni 15.
Crystal Palace pia wako kwenye mazungumzo ya kumsaini kipa wa Ipswich Bartosz Bialkowski. Klabu hiyo inataka zaidi ya pauni milioni 4 kwa mchezaji huyo wa miaka 30.
Liverpool wametupilia mbali mpango wa kumsaini wing’a wa Monaco Thomas Lemarbada baada klabu hiyo kuomba pauni milioni 90 kwa mchezaji huyo wa miaka 22.
Meneja wa Leicester Claude Puel anasema hana hofu kwa kundoka mwezi huu kwa mAlgeria Riyad Mahrez, 26.
AC Milan wanasema kuwa kuwa hawawezi kumuuza kiungo wa kati mHispania Suso 24, hata kwa pauni milioni 71.
Liverpool wapo tayari kupambana na Manchester City na Manchester United katika kutaka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 29.
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho yuko tayari kuacha kumsajili Antoine Griezmann, 26, kutoka Atletico Madrid mwisho wa msimu na hata Gareth Bale, 28, kutoka Real Madrid, ili amsajili Sanchez na kumpa mshahara wa pauni 350,000 kwa wiki.
Manchester United wamempa Alexis Sanchez hadi siku ya Ijumaa kuamua kama anataka kwenda Old Trafford au la, vinginevyo wataachana naye.