Mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez anakaribia kuhamia Paris St-Germain baada ya agenti wake kuelekea katika mji mkuu wa Ufaransa kwa mazungumzo.
PSG itajaribu kumsajili Sanchez kwa dau la £25m ijapokuwa Manchester City bado wanamtaka mchezaji huyo wa Chile baada ya kushindwa kumpata mchezaji huyo kwa dau la £60m katika dirisha la uhamisho lililiopita.
Sanchez atasalia Arsenal mwisho wa msimu na baadaye ajiunge na Manchester City katika uhamisho wa bure , mpango ambao utampatia kipato cha £400,000 kwa wiki.
Barcelona iko tayari kulipa £132m ili kumsajili kiungo wa kati wa Liverpool Philippe Coutinho, 25, katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari.
Bale ameichezea Real Madrid mara 12 pekee msimu huu na kufunga mabao manne.Je Jumamosi ijayo itakuwa mechi yake ya mwisho ya El Classico.
Atletico Madrid inasema kuwa beki Sime Vrsaljko, 25, anayelengwa na Liverpool, hataondoka mwezi ujao.
Chelsea huenda wakagonga mwamba kumsajili winga wa Bayer Leverkusen Leon Bailey, 20, mwezi ujao lakini bado wanamtaka kiungo wa kati wa Everton Ross Barkley, 24, na mshambuliaji wa Monaco Thomas Lemar, 22.
Arsenal na Liverpool wako katika mazungumzo ya kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Real Madrid Dani Ceballos, 21.
Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger anasema kuwa kuna uwezekano mkubwa wa asilimia 90 kwamba hataongeza mchezaji mpya katika kikosi chake mnamo mwezi Januari.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 amekuwa katika mkopo katika klabu hiyo ya Uhispania na amevutia Arsenal na Manchester United.
Arsenal na Manchester City zinamkagua beki wa Burnley James Tarkowski, 25, kwa lengo la kumvutia katika dirisha la uhamisho la mwezi ujao.
Mchezaji anayelengwa na Arsenal na Everton Steven N’Zonzi amedaiwa kuonekana katika uwanja wa ndege wa Gatwick.
Mchezaji huyo wa zamani wa Stoke na Blackburn 29, ameambia Sevilla kwamba anataka kuondoka.
Klabu hiyo pia imefanikiwa kumtia mkobani kwa mkopo winga wa Chelsea Kenedy, 21, na anatarajiwa kuwasili wakati dirisha la uhamisho litakapofunguliwa mwezi ujao.
Ajenti wa kiungo wa kati wa Juventus Stefano Sturaro’s anasema kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ambaye analengwa na Newcastle, huenda akahamia huko mwezi Januari.
Klabu hiyo hatahivyo inakabiliwa na pingamizi kutoka kwa klabu hiyo ya daraja la kwanza kumnyakua mchezaji huyo mwenye umri wa 24-year-old.
Kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere, 25, anasema kuwa anataka kusalia katika klabu hiyo na analenga kuichezea Uingereza katika kombe la dunia la 2018.
Liverpool itakataa katakata kumuachilia mshambuliaji Daniel Sturridge kuondoka mwezi Januari, na hivyobasi kuweka matumaini yake ya kutaka kuichezea Uingereza katika hali ngumu .
Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amempatia Ben Woodburn ruhusa ya kuondoka katika klabu hiyo kwa mkopo.
Mkurugenzi wa Inter Milan Walter Sabatini amesisitiza kwamba klabu hiyo haina nia ya kumuachilia Joao Mario, 24, kuondoka mwezi Januari.
Kipa Claudio Bravo, 34, amesema kuwa ana uhusiano mbaya na mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola lakini anasisitiza kuwa hana mpango wa kuondoka katika klabu hiyo hivi karibuni.