Klabu ya Chelsea wanakaribia kukamilisha usajili wa kiungo wa Monaco Tiemoue Bakayoko, 22, na huenda akasaini mkataba wake kabla ya Jumatatu na kusafiri na timu kwenda Singapore na China (Sky Sports).

Manchester United wanataka kupanda dau zaidi ya la Chelsea na kumsajili Tiemoue Bakayoko kwa pauni milioni 40 (Daily Mail).

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho pia anataka klabu hiyo kutoa dau la pauni milioni 60 ili kutaka kumsajili kiungo wa Tottenham Eric Dier 23 (Mirror).

Manchester United hawatomuongeza mkataba Zlatan Ibrahimovic, 35, licha ya kumruhusu kuendelea kutumia uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo wa Carrington wakati akiuguza jeraha lake la goti (Star).

Manchester United bado hawajaweza kutoa kiasi wanachotaka Inter Milan ili kumsajili winga Ivan Perisic, 28, lakini wanatazamia kukamilisha mkataba wa pauni kati ya milioni 45 hadi 50 (Independent).

Arsenal wana uhakika wa kutomuuza kiungo Alex Oxlade-Chamberlain, 23 ambaye amebakiza miezi 12 tu kwenye mkataba wake wa sasa (Daily Mail).

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger pia amedhamiria kutomuuza Alexis Sanchez, 28, ambaye hajasaini mkataba mpya na inadhaniwa anataka kwenda Manchester City (Independent).

Arsene Wenger hataki kumuuza Olivier Giroud, 30, mpaka suala la Alexis Sanchez na Thomas Lemar litakapotatuliwa (Daily Telegraph).

Arsenal watapambana na Liverpool katika kutaka kumsajili beki wa Southampton Virgil van Dijk, 26 (Sun).

Chelsea wameweka kipaumbele katika kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata, 24, huku kukiwa hakuna uhakika na hatma ya Diego Costa, 28 (Guardian).

Diego Costa yuko tayari kuichezea Chelsea na kufikia muafaka na meneja wake Antonio Conte (Star).

Roma wanataka kumchukua kwa mkopo mshambuliaji wa Manchester United Anthony Martial, 21, lakini Old Trafford huenda wakapinga hatua hiyo (Mirror).

Manchester City wapo tayari kutoa pauni milioni 27 kumsajili beki wa kati wa Real Sociedad Inigo Martinez, 26 (Marca).

Meneja wa Leicester amekuwa na mazungumzo na winga Demarai Gray, 21, na anataka mchezaji huyo asiondoke huku Liverpool, Tottenham na Everton zikimtaka (Sky Sports).

Leicester City wamekubaliana kimsingi na Manchester City kuhusu kumsajili mshambuliaji Kelechi Iheanacho, 20 (Sky Sports).

James Rodriguez, 26, anataka hatma yake ifahamike mara moja, huku Real Madrid wakitaka pauni milioni 62. Manchester United na timu kadhaa Ulaya zimeambiwa zinaweza kupanda dau (Mail).

Tottenham watakuwa na mazungumzo na Estudiantes wiki hii kuhusiana na usajili wa beki Juan Foyth, 19 (London Evening Standard).

Deportivo La Coruna hawana uhakika kama wataweza kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Lucas Perez, 28, msimu huu (FourFourTwo).

Burnley wanafikiria kumsajili kiungo wa Swansea Jack Cork, 28, lakini wamesema hawamtaki kiungo wa Stoke Glenn Whelan, 33 (Lancashire Telegraph).

Newcastle wanafikiria kumchukua kipa wa Paris Saint-Germain Alphonce Areola, 24 (France Football).

Newcastle watamkosa winga wa Manchester City Jesus Navas, 31, ambaye anakaribia kurejea Sevilla (Marca).

Meneja wa Newcastle Rafael Benitez ametaka klabu yake kuongeza dau katika kumsajili winga wa Norwich Jacob Murphy (Daily Telegraph).

Paris Saint-Germain wanasubiri kuona kama wamefanikiwa kumshawishi Dani Alves, 34, asiende Manchester City (Daily Mail).

Brighton wanataka kumsajili kiungo wa Chelsea Izzy Brown, 20 (Brighton & Hove Independent).

Chelsea wanajiandaa kutoa pauni milioni 70 kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata, 24 (AS).

Inter Milan watapambana na Manchester United kutaka kumsajili kiungo wa Chelsea Nemanja Matic, 28 (Corriere dello Sport).

Tottenham nao wanamtaka mshambuliaji wa Manchester City Kelechi Iheanacho, 20 (The Sun).

Everton wanafikiria kumchukua mshambuliaji wa Crystal Palace Christian Benteke kuziba nafasi ya Romelu Lukaku. Everton pia wanamtaka Olivier Giroud au Edin Dzeko (Daily Mail).

Manchester United walikataa nafasi ya kumsajili Alexandre Lacazette na badala yake wakaamua kumfuatilia Romelu Lukaku (The Guardian).

Dani Alves bado hajaamua aende wapi huku Manchester City, Chelsea na Tottenham zikimtaka (Globo Esporte).

Atletico Madrid wamekubaliana mkataba wa euro milioni 45 na Monaco wa kumsajili Fabinho ambaye amehusishwa na Manchester United, PSG na Manchester City, lakini huenda akajiunga na Atletico baada ya adhabu yao kumalizika (AS).

Liverpool bado wanavutana na mshambuliaji wa Atletico Madrid Angel Correa ambaye ada yake ya uhamisho ya pauni milioni 25 imekubaliwa lakini mchezaji huyu anataka mshahara mkubwa kuliko Liverpool wanaotaka kutoa (Foot Mercato).

Chelsea wanataka kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre Emerick-Aubameyang, 28, baada ya kumkosa Romelu Lukaku na wapo tayari kulipa euro milioni 70 (Marca).

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *