Tetemeko kubwa la ardhi la nguvu ya 8 katika vipimo vya richa limekumba pwani kusini mwa Mexico.
Kitovu cha tetemeko hilo lilitokea umbalia wa karibu milomita 100 kuisni magharibi mwa mji wa Pijijiapan katika kina cha kilomita 35, kwa mujibu wa idara ya hali ya hewa ya Marekani.
Onyo la kutoea tsumani limetolewa nchini Mexico, Guatemala, El Salvador, Costa Rica, Nicaragua, Panama na Honduras.
Tetemeko hilo lilisikika mji wa wa Mexico City ambapo watu walitoka manyumbani mwao kwenda barabarani.
Mgeni mmoja katika mji huo Luis Carlos Briceno, aliliambia shirika la Reuters, “sijawai kuwa popote pale ambapo ardhi ilisonga sana.”
Kimbunga hicho cha kiwango cjha kwanza kiko umbalia wa killomita 300 kusini mashariki mwa Tampico na kimepata kasi ya kilomita 140 kwa saa.
Vifo vinne viliripotiwa katika jimbo la Chiapa nchini Mexico karibu na kitovu na vingine viwili katika jimbo la Tabasco.