Mwanamuziki kutokea pande za Nigeria, Tekno Miles amethibitisha kupata mtoto wa kwanza na mpenzi wake, Lola Rae.
Tekno na mrembo huyo walitangaza kuachana miezi sita iliyopita wakati huo Lola akiwa mjamzito, kila mmoja alimwondoa mwenzake kwenye akaunti ya Instagram lakini kupitia ukurasa huo wa Tekno ameweka wazi kuwa amepata mtoto.
Inasemekana wawili hao walimaliza tofauti zao mapema kabla ya mrembo huyo kujifungua mwishoni mwa wiki iliyopita.
“Hatimaye tumefikia kilele, nina furaha kubwa kupata mtoto,” aliandika Tekno kwenye ukurasa wake wa Instagram, akiambatanisha na alama nyingi zenye upendo.
Mwanamuziki huyo ni moja ya wasanii wanaofanya vizuri nchini Nigeria kutokana na nyimbo zake kukonga nyayo za mashabiki zake.