Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezipiga faini zaidi ya milioni 65 kampuni tisa za simu nchini kwa kosa la kushindwa kukidhi baadhi ya vigezo vya ubora.
Mkurugenzi wa TCRA, Mhandisi James Kilaba alizitaja kampuni hizo kuwa Benson Informatics Limited Smart, Airtel Tanzania, Vodacom Tanzania, Zanzibar Telecom Limited Zantel.
Nyingine ni Mic Tanzania Limited, Tigo, Viettel Tanzania limited, Halotel, na Tanzania Telecommunications Company Limited, TTCL huku akizitaka kampuni hizo kuhakikisha zinatoa huduma bora.
“TCRA inawakumbusha watoa huduma wote wa mawasiliano nchini kuhakikisha mnatoa huduma zinazokidhi ubora wa sauti na upakuaji wa hali ya juu (Kudownload) pamoja na kufuata sheria za huduma ya mawasiliano ya mwaka 2011”.
Pia Mhandisi huyo alisema wataendelea kuwachukulia hatua wale wote watakaoshindwa kukidhi vigezo vya ubora wa huduma kama ilivyo agizwa.