Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa onyo kwa watumiaji wa kompyuta kutofungua viambatanishi wasivyovijua kwenye barua pepe zao.

Onyo hilo limekuja kufuatia tishio la kuwapo programu mtumishi (software) yenye virusi aina ya WannaCry.

Pia taasisi zimetakiwa kutunza data nje ya mtandao ili kuepuka athari endapo kompyuta zitashambuliwa na virusi hivyo, sambamba na kuhuisha mifumo ya ulinzi dhidi ya virusi.

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba amebainisha kuenea kwa programu mtumishi hiyo yenye virusi vinavyoathiri na kumzuia mtumiaji kufikia mafaili au mifumo, ama kwa kufungia mifumo ya screen au kuharibu faili kwenye kompyuta.

Amesema kuwa Kilaba alisema tishio la virusi WannaCry haliko kwenye kompyuta pekee bali pia kwenye simu za kisasa endapo utafungua kiambatanisho au link yenye virusi hivyo.

Pia amesema kuwa Kilaba alisema virusi WannaCry kinaharibu programu za kwenye kompyuta zilizopitwa na wakati au software zenye shida hususani Microsoft Server Message Block 1.0 (SMBv1) zilizotolewa mapema mwaka huu na Microsoft kama njia ya kuzuia mazingira magumu na watumiaji wa Microsoft wanaweza kuokoa kompyuta zao kwa kuweka njia za usalama.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *