Mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale-Mwiru amefariki dunia leo katika hospitali ya taifa Muhimbili.

Taarifa hizo zimethibitishwa na Mtoto wake Kinje Ngombale kuwa Baba yake amefariki usiku wa kumakia leo.

Kingunge Ngombale Mwiru ni ni mstaafu ambaye katika maisha yake toka ujana wake amelitumikia Taifa mpaka hata ngazi za juu kabisa kama vile kuwa Mkuu wa Mkoa, Mbunge na hata Waziri.

Ni mmojawapo wa vijana wa TANU enzi zao hizo, walioshiriki harakati za kuutafuta uhuru mpaka ukapatikana.

Yeye kingunge ndiye aliyekabidhiwa jukumu la kuzigawa kadi mia za kwanza kabisa za wana TANU baada ya TANU kuanzishwa ambapo, Bwana Sykes ndiye aliyezichapisha kwa pesa za kutoka mfukoni mwake.

Kingunge alifanya kazi akiwa karibu na Mwalimu Nyerere na waliendelea kuwa karibu hata baada ya uhuru kwa majukumu ya kujenga Taifa la Tanzania.

Kingunge alikuwa ni mmoja wa watu waliokuwa na nafasi nyeti katika TANU na CCM mpaka pale alipoamua kuondoka CCM wakati wa uchaguzi wa mwaka 2015 na kwenda upande wa upinzani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *