Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania, Sir George Kahama amefariki dunia jana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akiwa na umri wa miaka 88.

Kahama amefariki jana majira ya saa 10 jioni, huku maradhi yaliyosababisha kifo chake yakiwa bado hayajawekwa wazi.

Enzi za uhai wake, Kahama amewahi kuwa Waziri wa mambo ya Ndani wa Tanganyika (1961- 1962) na alikuwa msaidizi wa karibu wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Mara ya mwisho, Kahama alionekana kwenye majukwaa ya kisiasa akiwa na aliyekuwa akiwania kuteuliwa kugombea urais kwa tiketi ya CCM, Benard Membe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *