Tanzania imeshuka nafasi 12 kwenye orodha ya viwango vya ubora wa soka duniani baada ya kushika nafasi ya 144 huku Argentina ikishika nafasi ya kwanza kwenye viwango hivyo.

Ujerumani inashika nafasi ya pili huku nafasi ya tatu ikishiliwa na Brazil na nafasi ya nne ikishikiliwa na Ubelgiji

Kwa upande wa Afrika Uganda wamo nambari 72 baada ya kushuka nafasi saba, Kenya wamepanda nafasi sita hadi nambari 85 nao Rwanda wamesalia nambari 107.

Ethiopia wanashika nafasi ya 126 huku Malawi ikishika nafasi ya 100 pamoja na Burundi ikishika nafasi ya 138.

Mabingwa wa Afrika Ivory Coast wanashikilia nafasi ya 31 duniani kwa Afrika ikiwa ya kwanza wakifuatiwa na Senegal ambao wanashika nafasi ya 32 kwa Afrika ya pili.

Mabadiliko haya yamekuja hasa kwa kuzingatia Matokeo ya Mechi za kuwania kutinga Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Urusi.

Orodha nyingine ya Ubora wa viwango itatolewa Novemba 24 mwaka huu na Shirikisho la soka duniani FIFA.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *