Serikali ya Tanzania jana imepokea msaada wa fedha kutoka Umoja wa Ulaya (European Union) wenye thamani ya Sh. bilioni 490 kwa ajili ya kuboresha huduma za kijami.
Msaada huo umekabidhiwa na mwenyekiti wa umoja huo anayeshughulikia huduma za maendeleo ya kijamii na uchumi, Roeland Van de Geer .
Mwenyekiti huyo amesema kuwa sababu ya utoaji msaada huo ni kutokana na kuvutiwa na uongozi wa Rais John Magufuli kuhusiana na uendeshaji wa sera za kiuchumi na umakini.
Pia amesema msaada huo usiokuwa na masharti utafanyiwa utekelezaji bora katika mwaka wa bajeti unaoanza wa 2017/18.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dk. Dotto James, amesema anaushukuru umoja huo kwa msaada huo na akawahakikishia kwamba msaada huo utaelekezwa katika huduma za kijamii kama ilivyoelekezwa katika mkataba wao hasa katika masuala ya elimu, kilimo na sekta nyingine.
Msaada huo utagawanywa katika awamu nne ambapo kila mwaka wa fedha kitatolewa kiasi cha Sh. billion 120 cha fedha hizo.