Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imepanda kwa nafasi 25 hadi nafasi 114 kutoka nafasi ya 139 kati ya mataifa 211 katika viwango vya ubora wa soka duniani vilivyotolewa na Shirikisho la Soka Duniani FIFA leo.
Katika viwango hivyo vya mwezi Julai timu ya taifa ya Ujerumani inashika nafasi ya kwanza, Brazili ikishika nafasi ya pili, na timu ya Argentina ikishika nafasi ya tatu.
10 bora duniani zipo kama ifuatavyo
1.Ujerumani
24.Ureno
5.Uswisi
6.Poland
7.Chile
8.Colombia
9.Ufaransa
10.Ubelgiji
Barani Afrika Misri inaongoza ikiwa nafasi ya 24 ikifuatiwa na Senegal katika nafasi ya 27, Congo DR nafasi ya 28, Tunisia nafasi ya 34, Cameroon nafasi ya 36, Nigeria nafasi ya 39 huku Burkina Faso akiangukia nafasi ya 44.