Tanzania imesema imeshtushwa baada ya kuorodheshwa miongoni mwa nchi ambazo zimechunguzwa na Umoja wa Mataifa na kuhusishwa kuwa na uhusiano wa kibiashara na Korea Kaskazini.

Hayo yamesemwa leo na waziri wa mambo ya nje Dkt. Augustine Mahiga ambapo amesema licha ya uhusiano uliokuwepo awali, lakini tangu mnamo mwaka 2014 Tanzania imepunguza kabisa uhusiano wa kibiashara na kidiplomasia na nchi hiyo.

Waziri Mahiga ameongeza kusema kuwa uhusiano huo wa kibiashara ulikuwepo kabla ya vikwazo vilivyowekwa hivi karibuni na Baraza la Umoja wa Mataifa.

Pia Waziri huyo amesema anaelekea katika mkutano wa kawaida wa Umoja wa Mataifa, ambapo atatumia fursa hiyo kujibu tuhuma hizo kwa Baraza la Usalama.

Taarifa za hivi karibuni zilisema kuwa Umoja wa Mataifa inaichunguza Tanzania na Uganda kwa kuendeleza uhusiano na nchi ya Korea Kaskazini ambayo imewekewa vikwazo vya kiuchunu na Umoja wa Mataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *