Tanzania mwaka huu itakuwa miongoni mwa nchi zitakazoshiriki tuzo maarufu za filamu duniani za Oscars ambapo imepewa nafasi ya kushiriki katika kipengele cha filamu za nje ya Marekani (Foreign Film).

Hii ni baada ya nchi hiyo kukubaliwa kamati yake iliyoiunda ya kuchuja filamu itakayoshindanishwa katika tuzo hizo ambapo itahusisha filamu zilizotaka Januari Mosi, 2022 hadi Novemba 30, 2022.

Katibu Mtendaji wa bodi ya filamu, Dk Kiagho Kilonzo amesema mchakato wa kupendekeza kamati hiyo ulianza tangu mwaka 2019 na hatimaye imekubaliwa mwaka huu.

Dk Kilonzo aliwataja wajumbe wanaounda  kamati hiyo ambao wapo 10 kuwa ni pamoja na Dk Mona Mwakalinga ambaye ni Mwenyekiti wa kamati hiyo.

Wengine ni Simon Peter (Katibu), Profesa Martin Mhando, Single Mtambalike ‘Rich Rich’, Binay Gokan, Zamaradi Nzowa, Adam Juma, Daniel Menege, Florence Mkinga na Vyonne Cherie ‘Monalisa’.

Pia amesema amesema vigezo vya kushiriki kwenye tuzo ni pamoja na filamu iwe imetayarishwa nje ya Marekani.

“Pia iwe katika muundo wa Digital Cinema Package (DCP) kwa ubora angalau 2040 kwa 1080 pxels (2k), iwe na sauti ya kipimo cha 5.1 au 7.1 au iwe yenye chanel 3 za sauti (left, right and centre),” amesema Dk Mona.

Maonyesho hayo ni pamoja na cable televisheni, DVD, isiwe imeonyeshwa kwenye ndege na kwenye mtandao wa Internet.

Kamati hiyo inatarajia kupokea filamu hizo kuanzia Agosti 1 hadi Agosti 30, 2022 kupitia mtandao wa tanzaniaoscars@gmail.com.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *