Aliyekuwa mpenzi wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz aitwae Tanasha raia wa Kenya amefunguka na kusema kuwa hajisikii vibaya, Diamond akimuoa Zuchu.
Tanasha amesema kuwa yeye ajali baadala yake ameelekeza nguvu zake kwenye sanaa yake ya muziki.
Diamond na Zuchu wamekuwa wakizua gumzo toka Desemba, mwaka jana wakidaiwa ni wapenzi kutokana na ishara mbalimbali wanazozionesha.
Madai kwamba, wawili hao wanatoka kimapenzi yalichochewa na kitendo cha Diamond kumtoa Zuchu usiku katika Hoteli ya Serena jijini Dar.
Watu kibao wa Wasafi wakiongozwa na Mama Dangote, Romy Jons, Rayvanny na ‘machawa’ ndiyo wakaanza kuimba mapenzi ya Diamond na Zuchu.
Hata alipoulizwa Bi Khadija; mama wa Zuchu, naye akasema hakuna ubaya wakioana kwani siyo ndugu wa tumbo moja.
Madai hayo yalikwenda mbali zaidi ikielezwa kwamba, Diamond amepanga kumuoa Zuchu siku ya Valentine Februari 14, 2022.
Muda wote wakati sakata hilo likifukuta, ma-baby mama wa Diamond, Zari The Boss Lady, Hamisa Mobeto na Tanasha walikuwa kimya.