Mwanamuziki wa Kenya ambaye pia ni mzazi mwenza wa msanii Diamond Platnumz, Tanasha Dona amewasili nchini kiwa na mtoto wake wa miaka miwili aliyezaa na Diamond anayefahamika kama Naseeb Junior.
Tanasha ameingia nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ‘Terminal 3’ saa tatu usiku.
Hata hivyo Tanasha hakutaka kuwa rafiki wa maswali ya waandishi wala kamera zao ambapo alijibu kwa mkato kuwa amemleta mtoto kwa baba yake kisha akaomba asiulizwe maswali zaidi. Na hata waandishi walipoendelea kumuuliza, hakuonesha ushirikiano.
Ujio wa Tanasha unafafana na ule wa mzazi mwenza mwingine wa Diamond, Zari The Boss Lady ambaye alikuja nchini Novemba 5 mwaka jana akiwa na watoto wawili aliozaa na Diamond, Latifa maarufu Tiffah Dangote na Nilan huku sababu ikiwa ni kuwaleta kwa ajili ya kuonana na baba yao baada ya kutokukutana kwa zaidi ya miaka miwili.
Mbali na kumleta mtoto kwa baba yake, Tanasha Dona anahusishwa kuwa moja ya wasanii watakaoshambulia jukwaa la tamasha la Tumewasha Januari 30 Uwanja wa Uhuru.