Msimu wa Nne wa Tamasha la muziki la Ongala umerudi tena na litafanyakika kuanzia Tarehe 5 hadi 7, mwezi wa nane, kuadhimisha muziki, maisha na urithi wa Dr. Remmy Ongala (1947 – 2010), pamoja na ari na utamaduni wa watu wa Tanzania
Tamasha la muziki la Ongala lilioanzishwa mwaka 2018, ni tamasha la kipekee la siku tatu la muziki wa LIVE litakalofanyika tarehe 05, 06 na 07, mwezi wa nane, katika fukwe za hoteli ya Silver Sands, Kunduchi, Dar es Salaam.
Remmy Ongala alikuwa ni mwanamuziki mashuhuri na maarufu aliyejulikana na mashabiki zake kama mtu wa watu katika maisha yake.
Tamasha la Muziki la Ongala limejengwa katika hali ya maadili ya Remmy ya kuwawezesha, kuwalea na kuwasaidia wasanii kote barani Afrika. Tamasha hilo linalenga kutoa jukwaa la kimataifa kwa wasanii wa Kiafrika, ili kukuza mziki na kukua ndani ya bara lao huku wakilenga kufikia maono ya Remmy ya kuachanganya aina tofauti za sanaa na mitindo ya muziki.
Tamasha hili la ufukweni litajumuisha mseto wa wasanii wa ndani na wa kimataifa, ma DJ, waonyesha maonesho ya sanaa, soko la Chakula, warsha, ngoma, kutakuwa na nafasi ya kuweka kambi, malazi (Vyumba) vya hoteli vitapatikana na pia kutakuwa na warsha kwa wasanii ili kuongeza uelewa wao katika sehemu mbalimbali za sanaa ya mziki. Milango ya tamasha itafunguliwa kuanzia saa 4 asubuhi kila siku.
Miongoni mwa mada za warsha ni “Utunzi na Uandishi wa Nyimbo,” na “Jukwaa na stadi za Utendaji,” na moja ya warsha kuu ni Jukwaa la Ingoma, litakalokuwa linatumika kwa Jam Sessions na litakalosimamiwa na washirika wetu wa mara ya kwaza, Action Music Academy (AMA).