Tamasha la Nyege Nyege limepata mwanga wa kijani kutoka kwa serikali ya Uganda kuendelea kama ilivyopangwa.

Kulingana na Waziri Mkuu wa Uganda Robinah Nabbanja, hafla hiyo itaendelea lakini chini ya miongozo mikali iliyowekwa na Serikali.

Maagizo hayo yanakuja mara baada ya bunge la Uganda kufuta hafla hiyo kutokana na wasiwasi wa ukosefu wa maadili.

Mjadala wa Bunge la Uganda ulikuja baada ya Mbunge wa Tororo Sarah Opendi ambaye alisema kuwa tukio hilo ni chanzo cha uasherati.

“Bunge limesitisha tamasha la ‘Nyege Nyege’, hafla ya kila mwaka ya kijamii iliyopangwa kufanyika wiki ijayo huko Jinja. Mbunge wa Tororo Mwanamke Mhe Sarah Opendi anasema tukio hilo ni msingi wa uasherati,” bunge la Uganda liliandika kwenye Twitter.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *