Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize ameweka wazi kuwa tamasha lake la Afro East Carnival sasa itafanyika Julai 2 mwaka huu.
Kupitia akaunti ya mkurugenzi wa Media za EFM na TV E Majizo ameandika kuwa “Tumeshirikiana na Harmonize kuandaa Afro East Carnival.
Nampongeza sana Harmonize, yeye kama sehemu muhimu ya tukio hili amekamilisha kila alilotakiwa kufanya, na sisi wadau wengine tumefanya asilimia kubwa ya wajibu wetu.
Lakini binafsi nimetafakari tena, nimepata kiu ya kufanya jambo kubwa zaidi ya tulilokuwa tumepanga. Nimeona haja ya kuongeza vitu.
Nashukuru Konde amenielewa, tumaehirisha Afro East Carnival Tutafanya TAREHE 02/7.
Tunaomba radhi kwa kuwasubirisha ila ni kwamba nia njema zaidi.