Watu 11 wamefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumamosi wakiwemo maafisa wawili wa polisi katika mkanyagano kwenye uwanja wa michezo uliokuwa umefurika watu waliokwenda.
Uwanja wa Mashujaa ulisheheni kupita kiwango kinachotakiwa ambapo watu 80,000 walioujaza uwanja huo kwa ajili ya kushuhudia tamasha la Staa wa Congo, Fally Ipupa kwa mujibu wa waziri wa mambo ya ndani.
Waandishi habari wa Reuters wamefahamisha kwamba baadhi ya mashabiki wengine walijilazimisha kuingia kwenye eneo la watu maalum yaani VIP na maeneo mengine maalum yaliyotengwa katika uwanja huo.
Taarifa ya polisi imeonesha watu 11 wamefariki kutokana na kukosa hewa pamoja na mkanyagano na wengine 7 wamelazwa hospitali kwa mujibu wa tamko lililotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kongo, Daniel Aelo Okito.