Vazi lenye historia katika muziki wa hip-hop linapigwa mnada – taji hilo la kifalme lilivaliwa na msanii nyota Notorious B.I.G. wakati alipokuwa akipiga picha za nyimbo zake za mwisho.
Picha hiyo kwa jina Mfalme wa New York , kama ilivyojulikana imechapishwa katika majarida tofauti , kanda za muziki , tisheti, katika kuta na hata katika msururu wa filamu ya NetFlix kwa jina Luke Cage.
Ni miongoni mwa vitu vinavyopigwa mnada katika jumba la Sotheby, mchango wa muziki wa hip-hop ambao unashirikisha barua za mapenzi zilizoandikwa na Tupac Shakur akiwa na umri wa miaka 16.
Baadhi ya fedha ziliuzokusanywa kupitia vitu 120 vinavypigwa mnada zitatumika katika miradi ya kijamii mjini New York.
Biggie alivalia taji hilo siku tatu kabla ya kupigwa risasi hadi kufa mnamo tarehe 9 mwezi Machi 1997. Msani hyo wa muziki wa rap na mpiga picha wake Barron Claiborne waliitia saini wakati huo na Barron amekuwa akilimiliki tangu wakati huo.
Kifa hicho kilibadili umaarufu wa Biggie Small kuwa kama ule wa mtakatifu na mtu wa tabaka la juu katika jamii, na kuchukuliwa sio tu kama mfalme wa New York , lakini pia mfalme wa muziki wa Hip Hop na msanii mkubwa wa kizazi chake.
Jumba la mnada la Sotheby linataraji kwamba taji hilo la kifalme litakusanya kati ya $200,000 hadi $300,000.
Taji hilo linapendwa sana wakati huu ijapokuwa msimamizi wa nembo ya Biggie ambaye alikuwa naye wakati wa shambulio hilo , aliripotiwa kuwa na wasiwasi wakati huo ilipoonekana kufanana na mfalme wa Burger badala ya yule wa muziki wa hip hop.