Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imeibuka mshindi wa tatu katika michuano ya kombe la Cosafa baada ya kupata ushindi wa penati 4-2 dhidi ya Lesotho jana.
Mechi hiyo ilimalizika kwa mikwaju ya penati baada ya kumalizika kwa matokeo ya 0-0 ndani ya dakika 90.
Taifa Stars ilikuwa ya kwanza kupiga mkwaju wa penati uliopigwa na Shiza Kichuya ambapo alikosa penati hiyo baada ya kugongesha mwamba.
Kwa upande wa Lesotho walikosa penati mbili moja iligonga mwamba na nyinigne iliokolewa na golikpia wa Tanzania, Said Mohamed ‘Nduda’.
Wachezaji wa Taifa Stars waliofunga penati ni Simon Msuva, Himid Mao, Abdi Banda na penati ya mwisho ilipigwa na Alpha.