Mchezaji wa Pescara, Sulley Muntari ameondoa uwanjani baada ya refa kumpa kadi ya njano, alipolalamika kufanyiwa ubaguzi wa raingi na mashabiki wa Cagliari.

Kiungo huyo wa zamani wa Ghana mwenye umri wa miaka 32, alimuomba refa Daniele Minelli asimamishe mechi hiyo ya Jumapili.

Lakini badala yake refa alimpa kadi yaanjano dakika ya 89, hatua iliyosababisha mchezaji huyo wa zamani ya vilabu vya Portsmouth na Sunderland kupinga kuondoka uwanjani.

Kwa hasira aliwakabili mashabiki wa klabu ya Cagliari akisema kwa sauti. “Hii ni rangu yangu.”

Akiongea baada ya mechi Muntari alisema: “Refa hastahili kukaa tu uwanjani na kupiga firimbi, ni lazima afanye kila kitu.

Meneja wa Pescarfa Zdenek Zeman ambaye upande wake ulishindwa kwa bao 1-0, alisema kuwa alimuomba refa kuingilia kati lakini akasema hakuona wala kusikia chochote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *