Kesi ya Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga imeahirishwa kwa muda kabla ya washtakiwa kuanza utetezi wao baada ya kumkataa Hakimu Mfawidhi Michael Mteite kuendelea kusikiliza kesi hiyo.

Wakili anayewatetea washtakiwa Boniphace Mwabikusi amemwambia Hakimu Mteite kuwa washtakiwa wana jambo la kuongea ndipo waliruhusiwa na Mbunge Joseph Mbilinyi aliiambia Mahakama kuwa hana imani na Hakimu Mteite.

Joseph Mbilinyi ametoa sababu za kumkataa Hakimu na kusema “ameegemea upande mmoja na kuwanyimwa dhamana kinyume cha Sheria na Katiba, Hakimu kukiri kuwa kesi hii inampa shida huenda Hakimu anapata shinikizo hivyo hapendi apate shida.”

Naye Emmanuel Masonga ametoa sababu kumkataa Hakimu kuwa ni “Uamuzi wa kuvipokea vielelezo kama Recorder na kitabu cha maingizo (Register ), kitendo cha kukiri mbele ya wakili wa utetezi Boniphace Mwabikusi kuwa kesi hii inampa shida, hivyo ameona kuwa kuna shinikizo.”

Baada ya kutolewa sababu hizo za washtakiwa Hakimu Mteite ameahirisha kesi kwa muda wa saa moja atakapotoa uamuzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *