Sudan imekata uhusiano wake na Korea Kaskazini ili kutekeleza matakwa ya Marekani, ya kuondolewa vikwazo vya kiuchumi.

Marekani inatarajiwa kutangaza uamuzi wake ikiwa itaiondolea Sudan vikwazo ifikapo tarene 12 mwezi Oktoba.

Afisa wa cheo cha juu chini Sudan amesema kuwa walikuwa wametimiza matakwa yote na wanatarajia vizwazo hivyo kuondolewa.

Mwezi Julai rais wa Marekani Donald Trump, alihairisha uamuzi wake wa kuiondolea kabisa vikwazo Sudan kwa muda wa miezi mitatu.

Vikwazo vya kiuchumi vilitangazwa dhidi ya nchi hiyo baada ya ya kutajwa kuwa inayounga mkono ugaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *