Muigizaji wa Bongo Movie, Steve Mengere maarufu kama Steve Nyerere ameonyesha nia ya kugombea ubunge wa jimbo la Kinondoni.

Steve Nyerere amesema yeye ndiye kijana ambaye anakubalika zaidi katika wilaya ya Kinondoni hivyo anasubiriwa kugombea.

Amesema kuwa “Wilaya ya Kinondoni unapozungumzia vijana ambao ni ‘president’ ni Steve Nyerere, ndio maana jimbo la Kinondoni linanisubiri mimi, we pita kila sehemu uliza tu utaambiwa”.

Kutokana na hilo Steve Nyerere hatokuwa msanii wa kwanza kutangaza nia kwa jimbo la Kinondoni, kwani msanii wa muziki wa bongo fleva Khalid Mohamed maarufu kama TID, alishawahi kusikika akisema anakusudia kugombea ubunge wa jimbo hilo.

Jimbo la Kinondoni kwasasa lipo wazi kufuatia aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Khalid Mtulia (CUF) kujiuzuru na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *