Mchekeshaji maarufu Bongo Movie, Steve Nyerere amefunguka kuwa mwanamke anayemheshimu Bongo Movie kwa sasa ni Aunt Ezekiel pekee.

Steve alisema kuwa, anamheshimu kwa sababu ni mwanamke ambaye hajabweteka na amejitahidi sana kukusanya hela anazopata kufanya mambo ya maana kama alivyojenga nyumba maeneo ya Kigamboni tofauti na mastaa wengine.

“Yaani kwa kweli Bongo Muvi kwa wanawake nampa heshima kubwa Aunt,ni mdada ametulia na mzazi mwenziye amepata watoto lakini pia ameweza kujituma mpaka kujenga nyumba tofauti na wengine,”.

Muigizaji huyo amesema hayo baada ya kuona maendeleo yanayofanywa na muzigizaji huyo tofauti na waigizaji wengine wa Bongo Movie.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *