Muigizaji wa Bongo Movie, Steve Nyerere amekanusha taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kuwa msanii huyo anaumwa ugonjwa wa UKIMWI.

Steve Nyerere ambae wiki chache zilizopita alitangaza kuwa anaumwa sana na kwamba kama kuna mtu yeyote amemloga basi amsamehe kwa sababu maumivu hayo yamekuwa yakimtesa sana na kwamba mpaka sasa bado hajajua chanzo cha ugonjwa huo.

Muigizaji huyo amesema kuwa amesikia watu wakimuongelea na kusema kuwa anaumwa ukimwi lakini yeye kitu kinachomsumbua sio ukimwi bali ni maumivu ya mgongo na miguu inayomfanya kushindwa kuendelea na kazi zake.

Baadhi ya wanawake waliojitokeza katika mitandao ya kijamii siku za nyuma na kusema kuwa Steve Nyerere anaumwa ugonjwa wa ukimwi na kusema kuwa wanauthibitisho kwa sababu hata wao wameupata ugonjwa huo kupitia yeye,

Steve Nyerere hivi karibuni amekumbwa na tuhuma hizo na kusemekana kuwa amekuwa akiwasadia wasanii wachanga kwa kuomba kufanya nao ngono na kusababisha kuwaambiza uginjwa huo alionao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *