Muigizaji wa Bongo Movie, Steven Mangere maarufu kama Steve Nyerere amefunguka sababu ya kutojumuika kwenye maandamano na waigizaji wenzake katika mitaa ya Kariakoo kupinga uuzwaji wa CD za kigeni.
Steve Nyerere amesema kuwa hawezi kwenda kwenye maandamano hayo kwasababu kuzuia CD za kigeni si suluhisho la kuinua movie za Bongo kwasababu hazina ubora kama za kigeni.
Muigizaji huyo ambaye kwasasa amejikita kwenye Stand Up comedy amesema kuwa sababu ya yeye kutoungana na wasanii wenzake kuandamana ni kwa kuwa jambo hilo halioni kama lina tija kwake.
Steve amesema kuwa si kweli kama movie za nje zinauwa soko la ndani kwasababu zilikuwepo toka wanazaliwa akitolea mfano movie za Arnold Schweziniger na Rambo huku akisema zilikuwa zinauzwa Kariakoo.
Pia akasema kuwa waliwakuta wanaigeria pamoja na filamu za kihindi na wakashindana nao ndani na waliweza kuwashinda.
Aliongeza kwa kusema kuwa watanzania wamezoea kukaa mezani na siyo maandamano kama walivyofanya wasanii wenzake jana katika mitaa ya Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Steve aliendelea kusema kuwa kama kuzuia utazuia Dar es Salaam itakuaje mikoa mingine kama vile Arusha, Dodoma na Mwanza wakati janga sio la Dar es Salaam.
Mwisho amesema kuwa waigizaji wameshindwa kutengeneza radha ya Watanzania kutokana na hayo wasiwaadhibu wafanyabiashara wajiadhibu wao wenyewe kwa kutengeneza filamu zisizouza.