Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa adhabu kali kwa vituo vinne vya utangazaji kwa kukiuka maadili ya utangazaji kwa mujibu wa sheria na kuvitaka viombe radhi siku tatu mfululizo kuanzia jana kupitia taarifa ya habari.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Valerie Msoka amesema vituo hivyo vimepewa onyo kali ikiwa ni pamoja na kutozwa faini na kuomba radhi wasikilizaji wake.

Amevitaja vituo hivyo kuwa ni Star TV,Channel ten, Clouds FM na Times FM ambapo vimekiuka kanuni na taratibu za utangazaji.

Vituo hivyo vimeanza kutekeleza adhabu hiyo kuanzia jana kwenye vipindi vyao kama walivyoagizwa na mamlaka hiyo ya mawasiliano nchini kutokana na kukiuka sheria za utangazi.

Kwa upande wa Clouds Media adhabu hiyo inawakuta kwa mara ya pili baada ya mwaka jana kipindi chao cha cha Take One kufungiwa kutokana na kukosa maadili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *